Alhamisi 21 Mei 2026 - 22:13
Wote wanapaswa kufuata maamuzi ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi/ Tunawashukuru sana wananchi kutokana na mikusanyiko ya usiku

Hawza/ Mtukufu Ayatullah Nouri Hamedani, huku akitoa shukrani na pongezi kwa mshikamano wa kitaifa na ushiriki mkubwa wa wananchi katika mikusanyiko ya usiku, alisisitiza: Kila jambo ambalo Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ataamua, ni wajibu kwa watu wote kulitii; uamuzi huo uwe katika medani ya mapambano au katika uga wa diplomasia.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Muhammad Qomi, mkuu wa Shirika la Tablighi nchini Iran, alikutana na kufanya mazungumzo na Mtukufu Ayatullah Nouri Hamedani.

Mtukufu Ayatullah Nouri Hamadani katika mkutano huo, sambamba na kutoa shukrani na pongezi kwa juhudi na kazi za Shirika la Tablighi, huku akirejelea ushiriki mkubwa wa wananchi katika mikusanyiko ya usiku, alisisitiza umuhimu wa kuimarishwa kwa uwepo huo na akasema: Sisi tunathamini uwepo wa wananchi, na kadiri uwepo huu unavyokuwa mkubwa zaidi, ndivyo uungaji mkono madhubuti zaidi kwa mfumo, Mapinduzi na uongozi mkuu utakavyoundika.

Marjii huyu wa taqlidi, huku akisisitiza juu ya kuhifadhi umoja na mshikamano wa kitaifa, aliongeza kuwa: Mikusanyiko hiyo ni lazima itekelezwe kwa namna ambayo hata chembe ya harufu ya hitilafu isiwepo, na isisikike isipokuwa sauti ya umoja, nayo ikiwa ni kuzunguka mtazamo wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi; na kila jambo ambalo yeye ataamua, ni wajibu kwa wote kulitii; uamuzi huo uwe katika medani ya mapambano au katika uga wa diplomasia.

Mwisho, mtukufu huyo alisisitiza kwa kusema: Wote tunapaswa kuwa na umoja, na sisi pia tunatoa shukrani na pongezi kwa mshikamano huu na uwepo mkubwa wenye hamasa wa wananchi.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha